27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Wakimbizi wa Sudan Kusini wakimbilia DRC

KINSHASA, DRC

UMOJA wa Mataifa (UN) juzi ulisema maelfu ya watu wanaokimbia ghasia Sudan Kusini wamevuka mpaka kuingia kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa taarifa ya ujumbe wa askari wa kulinda amani  Kongo (MONUSCO), wakimbizi wapatao 5,000 wamewasili katika vijiji vya mpakani karibu na mji wa Ingbokolo.

Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka Sudan mwaka 2011, na kuwa mwanachama wa 193 wa UN.

Lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka mwaka 2013 baada ya Rais Salva Kiir kumshutumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar, kujaribu kufanya mapinduzi ya  jeshi dhidi yake.

DRC inawahifadhi wakimbizi wapatao nusu milioni kutoka Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Lakini pia yenyewe ina wakimbizi 800,000 wanaotafuta hifadhi nje ya nchi hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles