32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

China yazindua App inayotambua mtu mwenye madeni

MWANDISHI WETU NA  MASHIRIKA

SERIKALI ya China imetengeneza app ambayo ina uwezo wa kumfahamisha mtu kuwa alipo kuna mtu mwenye madeni.

Gazeti la serikali, China Daily, lilitangaza kuwa maafisa wa mkoa wa Hebei waliunda app hiyo inayokwenda kwa jina la ‘map of deadbeat debtors’, ambayo inapatikana kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat, unaotumika katika taifa hilo.

Inavyofanya kazi app hiyo ni kuwa inaanza kuwaka wakati ikiwa umbali wa mita 500 na mtu aliye na madeni, gazeti hilo lilidai.

Vilevile, inaashiria mahali halisi alipo mdaiwa, ijapokuwa haikuwa wazi iwapo pia inaeleza taarifa binafsi kumhusu mdaiwa kama vile jina lake, picha na utambulisho mwingine.

Ikidaiwa kuwa inayolenga kuwafanya watu wawe macho na wenye madeni, bado haijafafanuliwa vyema iwapo kuna kiwango cha chini cha deni, ambacho app hiyo humulika.

Gazeti la China Daily lilisema app hiyo itawafanya watu kuwaanika watu wenye madeni, ambao wana uwezo wa kuyalipa.

Katika utamaduni wa China, kuweka hazina hutiliwa maanani kuliko kutumia fedha, huku kukopa na kurundika madeni kukiwa mwiko.

Mfumo huo mpya nchini China, ambao utaanza kazi mwaka ujao utakua ukikagua mtu kuhusu kiwango chake cha uaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles