Damian Masyenene, Mwanza
NI wazi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL), JKT Queens ya Dar es Salaam wana kikosi bora baada ya kuanza michezo yake minne bila kupoteza wala kuruhusu wavu wake kuguswa.
Katika michezo minne ya ligi hiyo iliyoanza Desemba 29, mwaka Jana, JKT Queens wameshinda michezo yote wakifunga mabao 40.
Wafungaji wa mabingwa hao watetezi waliobeba ubingwa msimu uliopita bila kupoteza hata mchezo mmoja kwenye mechi 14, wanachuana kufumania nyavu wakiongoza msimamo wa wafungaji kwa sasa.
Mshambuliaji wake, Fatuma Mustapha anaongoza akiwa amepachika mabao 17 kwenye mechi nne, akifuatiwa na Asha Rashid mwenye mabao 13 na kwa mbali wakifukuziwa na Aisha Khamis wa Alliance Girls ya Mwanza aliyepachika mabao Saba.
JKT Queens wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 12, wakifuatiwa na Mlandizi (10), Simba Queens (10), Panama (9), Alliance (7), Sisterz (7), Yanga Princess (6), Marsh Girls (5), Evergreen na Mapinduzi wote wakiwa na alama moja kila mmoja na wanaoburuza mkia ni Baobab Queens ya Dodoma pamoja na Tanzanite Queens ya Arusha ambao hawana alama yoyote.
Huu ndiyo Msimamo wa Wafungaji katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara
- Fatuma Mustapha (JKT)- 17
- Asha Rashid (JKT) – 13
- Aisha Khamis (Alliance) -7
- Amina Ramadhan (Simba) -6
- Mwantumu Ramadhan (Panama) -5
- Donisia Minja (JKT) -5
- Jamila Kassim (Mlandizi) – 5
- Asha Hamza (Sisterz) -4
- Mgeni Kisoda (Panama) -4
- Stumai Abdallah (JKT) -4
- Nasra Manduta (Panama) -3
- Mwanahamisi Omari (Simba) -3
- Vumilia Maarifa (Sisterz) -2
- Zainabu Mohamed ‘Dudu’ (Mlandizi) -2
- Stumai Abdallah (JKT) – 2
- Halima Mwaigomole (Panama) -2
- Aisha Juma (Alliance) -2
- Aisha Juma (Yanga) – 2
- Fatuma Iddy (Mlandizi) -2