33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Japan yajivunia mkataba wa amani na Urusi

TOKYO, Japan

WAZIRI Mkuu wa nchi hii, Shinzo Abe  amesema kwamba mkataba wa amani kati ya Serikali ya hapa na ya Urusi utaleta matokeo mazuri  juu ya usalama katika Ukanda wa  Asia na Pacific na pia utakuwa na manufaa kwa Marekani ambao walisaini  makubaliano ya usalama na Tokyo.

Waziri Mkuu huyo Abe alitoa kauli hiyo jana mjini hapa katika mahojiano na Kitu Cha Televisheni cha  NHK TV wakati akibu swali kuhusu mtazamo wake endapo mkataba huo utasainiwa.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Abe alisema kwamba mkataba wa Usalama wa Marekani na nchi hii ni msingi wa dhamana za usalama kwa taifa hili.

“Mkataba wa Usalama wa Japan  na Marekani ni msingi wa dhamana za usalama wa taifa la Japan,” alisema Waziri Mkuu Abe.

“Na hatimaye utakaposainiwa  mkataba wa amani kati ya Japan  na Urusi utakuwa na matokeo mazuri juu ya utulivu wa kikanda .. Nadhani hii itakuwa faida pia kwa Marekani,”aliongeza waziri mkuu huyo.

Alisema kwamba kiuhalisia Urusi inashikilia visiwa vinne kikiwamo cha  Kuril Kusini ambacho ili umuliki ake uweze kurejeshwa kwa Japan yanatakiwa kufikiwa makubaliano kupitia mkataba huo.

“Kuna mambo ambayo tumeyapendekeza ili kutatua tatizo hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili,”alisema Waziri Mkuu Abe.

 Waziri Mkuu huyo alifafanua kuwa pia mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa haya mawili,  Taro Kono wa Japan na  Sergey Lavrovwa Urusi watakutana mjini  Moscow Januari  14 mwaka huu kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles