30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Uchunguzi benki zote waanza kutoa jasho wafanyakazi

Na WAANDISHIWETU – DAR ESSALAAM

KAULI aliyoitoa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga, kwamba wako mbioni kuanza ukaguzi wa wafanyakazi wa benki zote nchini, ni kama imeanza kuwatoa jasho wafanyakazi hao.

Picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti dada la hili – MTANZANIA Jumamosi lililotoka jana, ambalo lilibeba habari hiyo ikimkariri Profesa Luoga ikiwa na kichwa kikubwa cha habari  ‘Uchunguzi mkubwa benki zote nchini’, ilikuwa ikitumiwa na wafanyakazi hao kusambaziana kupitia mitandao ya kijamii.

Waandishi wa gazeti hili wamedokezwa kuwa mijadala iliyoonekana kutawala zaidi katika makundi ya mitandao ya kijamii inayotumiwa na wafanyakazi wa benki mbalimbali, ni ile iliyohusu uchunguzi huo.

Juzi Profesa Luoga akizungumza na waandishi wa habari za uchumi jijini Dodoma, alisema lengo la hatua hiyo ni kupata wafanyakazi wakiwamo wakurugenzi wa benki hizo waliowaaminifu na watakao kuwa na uwezo wa kulinda fedha za wateja wadogo.

Alisema BoT imebaini huko nyuma fedha za wateja wadogo zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye baadhi ya benki ziliibwa kwa njia za ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jamboambalo ni kinyume cha sheria.

“Ili uwe kiongozi mzuri kwenye benki, lazima uwe mwaminifu na ndiyo maana BoT sasa unakwenda kufanya uhakiki wa benki zote nchini. Kwa maana hiyo hii ‘Staff Auditing’ (Ukaguzi wa wafanyakazi) sasa tutakwenda kupata wafanyakazi sahihi ambao watakuwa waaminifu na wakati wote watalinda fedha ya wateja na si hilo tuna hili tutalifanya hata kwa viongozi ambao wataongoza benki hizo.

“Na hawa ambao tutawafanyia ‘vetting’ ni lazima wahakikishe wanadhibiti vitendo ambavyo vinajenga picha mbaya kwa wananchi dhidi ya benki. Huko nyuma umefanyika ujanjamwingi, unaona taarifa kuwa aliyekopa anamiliki ghorofa, lakini ukienda kwenye nyumba unakuta ipo katikati ya mto. 

Kwa habari zaidi nakala yako ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles