27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vyuo vya elimu ya juu vyaendelea kumenyana Moshi

SAFINA SARWATT, MOSHI

Mashindano ya vyuo vya elimu ya juu (SHIMIVUTA) yameendelea kutimua vumbi leo Desemba 15 katika viwanja vya chuo Kikuu cha Ushirika  mkoani Kilimanjaro.

Katika Mashindano hayo timu ya mpira wa miguu kutoka chuo cha Mipango imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Chuo cha Ustawiwa Jamii.

Mabao ya chuo hicho yamefungwa kunako dakika 81 na dakika 94 huko bao la kufutia machozi la chuo cha Ustawi likifungwa dakika ya 45.

Kwa upande wa mpira wa pete Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeifunga timu ya Chuo cha DIT, mabao 35 kwa 12, huku Chuo cha LGTT ikikifunga Chuo cha MUST mabao 30 kwa 17.

Katika mchezo huo pia Chuo cha Mipango kimekivurumisha Chuo cha TIA mabao  28 kwa 19 na Chuo Mwalimu Nyerere kimeibugiza mabao 36 kwa 17 timu ya Chuo cha CBE huku IFM ikiivurumisha mabao 34 kwa 18 Chuo cha Maji.

Na katika mpira wa Wavu Chuo cha Nyerere kimekiadhibu  Chuo cha Ustawi kwa seti 3 kwa 2.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles