26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanaoishi na VVU 20,000 waacha kutumia ARV’S

DERICK MILTON na HARRIETH MANDARI  GEITA

ZAIDI ya watu 20,000 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi katika Mkoa wa Geita na walianzishiwa dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo (ARV’s) katika vituo vya kutolea huduma za tiba na matunzo (CTC) wanadaiwa kupotea.

Kupotea watu hao kunahatarisha ongezeko la maambukizi mapya ya   Ukimwi katika mkoa huo kwa vile haijulikani  wako wapi ikizingatiwa  wamekuwa hawahudhurii  kwenye vituo hivyo kwa muda mrefu.

Miongoni mwa  sababu kubwa inayofanya watu hao wapotee ni shughuli za uchimbaji, kilimo na uvuvi zinazowafanya kuhamahama huku wengine wakidaiwa kudanganya majina  wanapohamia maeneo mengine na hivyo kutoendelea na matibabu.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Ukimwi mkoani humo, Dk. Michael Kibaba, alipozungumza na  waandishi wa habari mjini Geita katika siku yatatu ya mafunzo kwa wanahabari kutoka kanda ya ziwa juu ya umuhimu wa toharakwa wanaume yaliyoendeshwa na Shirika la IntraHealth International.

Dk. Kibaba alisema   kuanzia mwaka 2013 hadi Septemba, 2018 wateja 74,077 waliandikishwa kwenye vituo hivyovya tiba na matunzo na kati ya hao 66,042 ndiyo walianzishiwa dawa za ARV’s.

Alisema   licha ya kuanzishiwa dawa watu 66,042 kwa kipindi hicho wanaoendelea na matibabumpaka sasa  ni 41,166 huku 24,876 wakidaiwa kupotea kusikojulikana na hawapo kwenye matibabu.

“Kwenye vitabu vyetu vya mahudhurio ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wameendelea kuja kliniki kwa ajili ya kuchukua dawa  ni 66, 042 nazaidi ya 20,000 hawajulikani walipo na wamepotea,” alisema Dkt Kibaba.

  Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt Japhet Simeo alisema  kwa   miaka miwili tangua 2017 hadi 2018 asilimia 70 ya watu waliogundulika kuwa na virusi vya Ukimwi wengi wao wamepotea.

Dk. Simeo alisema  katika kupambana na hali hiyo  wameweka mikakati ya kuhakikisha watu hao wanarejeshwa kwenye matibabu  kwa kushirikiana na kamati za afya wilaya hadi vijijini.

“Mkoa wa Geita umezungukwa na shughuli nyingi za uchimbaji wa madini, lakini pia kuna shuguli za uvuvi na kilimo, wengi wanahama kwenda kufanya kazi hizo  na wakifika uko hawaendelei na matibabu lakinipia wengine wakiendelea wanaamua kubadilisha majina,” alisema Dkt Simeo.

Alisema katika kupambana na ugonjwa huo ambao umepanda kutoka asilimia 4.5 mwaka 2016/17 hadi kufikiaasilimia tano mwaka 2018, wameanzisha kampeni ya Tohara Kinga kwa wanaume kwa kushirikiana na Intra Health International.

“Tumeweza  kuwafanyia tohara wanaume 115,000 sawa naasilimia 95, kati ya wanaume 119,000 ambao walilengwa kufanyiwa katika kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi Septemba, 2018.

“Mafanikio hayo tumeshirikiana na IntraHealth International kwa ufadhili wa mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Ukimwi ,” alisema Dkt Simeo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles