25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Kijaji asimamisha mfanyakazi TRA

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma



NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika ofisi ya mamlaka hiyo Mkoa wa Dodoma,Daniel Kingu  ili kupisha uchunguzi  kutokana na  tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja jijini humo.

Dk. Kijaji, alitoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mitaa ya Jiji la Dodoma jana,  baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee Sh 700,000 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFDs) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aende ofisini kwake chumba namba fulani, anafanya haya mambo ndani ya ofisi ya Serikali, akitoka nje inakuwaje? alihoji Dk. Kijaji.

Alisema hatasita kuchukua hatua hizo kwa wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo popote wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Aliwataka watendaji wa TRA  kufanyakazi zao kwa kuzingatia maadili yao ya kazi, kukadiria kodi kwa haki,  watumie lugha nzuri kwa wateja wao na kutoa elimu kwa umma kuhusu haki na wajibu wa wafanyabiashara katika masuala ya kodi badala ya kuwakadiria kodi kubwa isiyolipika.

“Ni lazima tuwalee wafanyabiashara hawa wadogo na ndio watakaotulipa kodi kubwa huko mbeleni badala ya kuwaumiza tangu wanapoanza biashara zao na ni lazima tuangalie viwango vyetu vya kodi tunavyotoza” Alisisitiza Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Thomas Masese aliahidi kutekeleza maagizo hayo na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo, huku  akiwaomba watumishi wa mamlaka hiyo  kufanyakazi zao bila kuwanyanyasa wafanyabiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles