27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

SIMBA, MTIBWA ZAKAMILISHA MIKAKATI YA USHINDI

Na MOHAMED KASSARA, DAR ES SALAAM


WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Kombe la Shirikisho la Afrika, Mtibwa Sugar, zinatarajia kuondoka nchini leo kwenda Shelisheli na Lesotho kwa ajili ya michezo yao ya marudiano dhidi ya timu za Northern  Dynamo na Mbabane Swallows.

Simba itaumana na Mbabane Swallows, katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Desemba 4, jijini Mbabane nchini Uswatini (zamani Swaziland), wakati Mtibwa itakabiliana na Northern Dynamo ya Shelisheli.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba 28, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows.

Ili kusonga mbele, Wekundu hao wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote.

Kama itafanikiwa kuing’oa Mbabane, Simba itatinga raundi ya kwanza na kukutana na mshindi kati ya Nkana Red Devils  ya Zambia na UD Songo ya Msumbiji.

Mshindi wa jumla katika mitanange miwili ya nyumbani na ugenini, atatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

Simba ilitarajia kuondoka na msafara wa watu 30, wakiwamo wachezaji 21.

Kwa upande mwingine,  Mtibwa  Sugar itashuka dimbani kuikabili Northen Dynamo, mchezo utakaochezwa Desemba 5.

Kikosi cha Mtibwa kinatarajia kuondoka leo saa 10 jioni, kikiwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi watano.

Mtibwa  ilizindua kwa kishindi kampeni za Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya  kuitandika Northen Dynamo ya Visiwa vya Shelisheli  mabao 4-0 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam

Wakata Miwa hao wakivuka kizingiti hicho, watakutana na KCCA ya Uganda.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuber Katwila, alisema ushindi mnono walioupata nyumbani hauwafanyi wawadharau wapinzani wao, badala yake wanakwenda Shelisheji wakiwa na ari ya kutaka kupata ushindi mwingine ugenini.

“Tulianza vema na matokeo mazuri nyumbani, lakini hilo halina maana kwamba tumeridhika na matokeo, mpira unabadilika wakati wowote.

Tunakwenda na tahadhari kubwa sana ya kutokukubali kufungwa ugenini,” alisema Katwila.

Naye kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems, alisema wanakwenda Swaziland wakifahamu kwamba watakutana na  mchezo mgumu kwavile wapinzani wao watakuwa nyumbani, lakini wamejipanga kwa ajili ya  kupata matokeo mazuri na kusonga mbele.

“Tunawafuata wapinzani wetu tukifahamu kwamba tutakuwa ugenini, nimewaambia wachezaji wangu waelewe kazi haijaisha, lazima wajiandae kwa mapambano.”

“Mashabiki wa Simba  na Watanzania wanataka matokeo mazuri, hivyo basi lazima tukawakabili wapinzani wetu  tukiwa na fikra za kuwakilisha taifa,”alisema kocha huyo raia wa   Ubeljigi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles