26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vigogo watano Wizara ya Ardhi wasimamishwa  kazi

Na Mwandishi Wetu-Dar es salaam

WIZARA  ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imewasimamisha kazi watumishi wake watano  kutokana na tuhuma zinazohusiana na vitendo vya utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili.

Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo iliwataja waliosimamishwa  kazi kuwa ni Dk. James Mtamakaya  ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani na Constantino Magambo ambaye ni Fundi Sanifu Mkuu 1 (Ramani).

Wengine ni Pascalia Mwitamba ambaye ni Fundi Sanifu Mkuu 1 (Ramani), Isack Marwa (Mpima Ardhi Mkuu) na Anorld Kamala ambaye ni Afisa Mipangomiji Mwandamizi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo watumishi hao walisimamishwa kazi tangu Novemba 26 mwaka huu ili  kupisha uchunguzi.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu waziri wake, William Lukuvi kutangaza maamuzi kadhaa ikiwa ni pamoja na kuvunja idara ya ardhi ya Jiji la Dar es Salaam  na kuagiza watumizi wote wa idara hiyo kuhamia wizarani.

Lukuvi alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za jiji hilo na kufanya ukaguzi katika masijala na kueleza kuwa msingi wa matatizo mengi ya ardhi Dar es salaam ni idara hiyo.

Mbali na hilo Lukuvi pia alitangaza msako wa nyumba kwa nyumba katika jiji la Dar es Salaam wenye lengo la kubaini wamiliki waliowahi kuwasilisha maombi ya hati katika wizara hiyo na kushindwa kuzichukua kwa miaka mingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles