25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 60 ya Watanzania bado wanatumia tiba asili

NA VERONICA ROMWALD- DAR ES SALAAM



 

ASILIMIA 60 ya watanzania bado wanategemea huduma ya tiba asili na tiba mbadala katika kutibu magonjwa mbalimbali na  wengi huanzia huko kabla ya kuanza matibabu ya kisasa hospitalini.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Msajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk. Ruth Suza, alipokuwa akiwasilisha mada katika semina ya siku moja iliyolenga kuwapa uelewa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya baraza hilo na hatua za usajili wa waganga wa tiba asili na mbadala.

“Takwimu hizi ni kwa mujibu wa tathmini ya Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa pia takriban asilimia 49 ya wajawazito wanajifungulia kwa wakunga wa jadi,” alisema.

Alisema hiyo ni wazi kwamba tiba asili ina mchango mkubwa katika afya na  uchumi kwa taifa.

“Kwa kutambua umuhimu na mchango wake, Serikali iliamua kurasimisha rasmi huduma hizi.

“Hadi kufikia mwaka 2017 waganga wa tiba asili na mbadala 19,942 wamesajiliwa, vituo 269 vimesajiliwa na tumepokea maombi mapya 1,350 ya usajili wa waganga,” alisema.

Alisema kati ya waganga hao watatu walifutiwa usajili kwa sababu walikiuka kanuni za baraza, wawili walipewa onyo kwa miezi sita na wawili walipewa onyo kali.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Edmund Kayombo, alisema kati ya waganga hao waliosajiliwa alikuwa namba moja kujisajili hata hivyo hakuweka wazi iwapo dawa yake maarufu ya kikombe cha babu imesajiliwa au la.

Naye, Mratibu wa Taifa wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Liggyle Vumilia alisema serikali inatambua mchango wa tiba hizo na inakusudia kuzipandisha hadhi.

“Tunatamani ifike wakati zitumike katika kutoa tiba hospitalini kama ilivyo China, tayari tumepata eneo la ekari 125  huko Kisarawe, mkoani Pwani ambako kitajengwa kituo kikubwa cha utafiti.

“Kutakuwa na ofisi zote zinazohusika kuanzia katika masuala ya utafiti wa mimea hadi usajili wa waganga hao, vituo vyao na dawa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles