Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, amemteua Meja Jenerali, George Msongole, kusimamia zoezi zima la kuhamisha korosho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Yacoub Mohamed, amesema Meja Jenerali Msongole atakuwa na timu yake.
“Mkuu wa Majeshi alitengeneza utaratibu wa kazi itakavyofanyika na alimteua Meja Jenerali, Msongole ambaye atakuwa na timu yake ambayo tayari iko hapa,” amesema Luteni Jenerali, Mohamed.
Tayari magari kadhaa ya JWTZ yatakayosomba korosho hizo yamewasili mkoani Mtwara.
Magari hayo yatasomba korosha kutoka kwenye maghala makuu na kuzipeleka katika maeneo maalumu yaliyoandaliwa kusubiri shughuli ya ubanguaji.