Dawasa yawataka wakazi wa Manzese, wachangamkie kuunganishiwa maji

0
1579

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Wakazi wa kata za Magomeni Manzese wametakiwa wajitokeze kwa wingi Ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa ) ili waunganishiwe huduma ya maji.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Dawasa, Neli Msuya amesema eneo hilo kwa sasa lina maji ya kutosha ndiyo maana wanawaasa wananchi wachangamkie fursa hiyo.

Amesema kuongeza kwa maji kunatokana na kukamilika kwa ulazaji wa bomba kubwa lenye ukubwa wa inchi sita.

“Tuna vifaa vya kutosha ambavyo kwa sasa vina uwezo wa kuunganisha zaidi ya wateja 2,000 katika Kata ya Manzese,” amesema Neli.

Dawasa inaendesha kampeni maalumu ya ‘DawasaTunawaitaji’ ikiwa na lengo la kuwarudishia maji wateja wake waliokatiwa kutokana na kushindwa kulipa ankara zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here