32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa sababu tisa kubana ‘vicoba,

Na FREDY AZZAH-DODOMA


SERIKALI imetoa sababu tisa za kutungwa  Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018.

Imesema  mojawapo   ni mwarobaini kwa watu wanaotoza riba kubwa ya mikopo ya kuanzia asilimia tatu mpaka 20 kwa mwezi ambayo ni sawa na asilimia 36 mpaka 240 kwa mwaka.

Akisoma muswada huo kwa mara ya pili bungeni jana , Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philp Mpango, alisema sekta ndogo ya fedha inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwamo viwango vikubwa vya riba za mikopo ambavyo havina uhalisia.

Alisema hali hiyo pia imesababisha kukosekana   masharti ya mikataba ya mikopo na kuwapo  masharti magumu ya kuilipa.

Alisema pia kumekuwa na mianya ya utakatishaji fedha haramu kutokana na taasisi za huduma ndogo ya fedha kutokuwa na utaratibu wa sheria unaozitaka kutekeleza matakwa ya Sheria ya Udhibiti wa Utakatishaji wa Fedha Haramu.

Dk. Mpango alisema pia kukosekana kwa sheria hiyo  kunafanya kusiwepo takwimu na taarifa sahihi za uendeshaji za watoa huduma ndogo ya fedha jambo linalofanya serikali kutojua mchango wa sekta hiyo.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni   kuwapo   baadhi ya taasisi ambazo hazitowi gawio au faida kwa wanachama, baadhi wananchi kuibia watu kupitia mitandao na majina ya viongozi, utaratibu mbovu wa kukusanya madeni na utoaji holela wa mikopo unaosababisha limbikizo la madeni kwa wateja.

Kutokana na hali hiyo, alisema sheria hiyo sasa itasaidia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa na mamlaka na jukumu la kusimamia sekta ndogo ya fedha, kuwalinda watumiaji wa sekta hiyo, kusimamia masharti ya utoaji wa riba na gawio kwenye hisa.

Wakichangia mswada huo, Mbunge wa Viti Maalimu Upendo Peneza (Chadema), alisema sheria hiyo inagusa watu wa chini   ambao wengine hawajui hata kuandika hivyo utawarudisha nyuma.

Alisema watu hao ambao wengi ni wanawake, kwa wiki ama mwezi hujichangishana  Sh 500 mpaka Sh 1,000 hivyo kusema lazima wajisajili, kutawakwaza wengi.

Mbunge wa Nzega Mjini,  Hussein Bashe (CCM), alisema kwa mujibu wa Seria ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha, suala la fedha ni la muungano hivyo Serikali iangalie namna ya kuweka sheria hiyo pamoja na ya Zanzibar ili huko mbele zisije kuleta shida.

Alimtaka pia Dk. Mpango akishatunga kanuni za sheri hiyo, azipeleke kwenye Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo  ipitiwe.

Mtolea alitangaza uamuzi huo bungeni Dodoma jana   baada ya Spika wa Bunge, Job

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles