25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Putin, Trump kukutana Argentina

MOSCOW, URUSI



RAIS Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani,  Donald Trump wanatarajia kuwa na mazungumzo nje ya mkutano wa mataifa makubwa 20 (G20) unaotarajiwa kufanyika nchini  Argentina mwishoni mwa mwezi huu.

Msemaji wa rais, Dmitry Peskov aliviambia vyombo vya habari juzi mjini hapa kwamba miongoni mwa watakayojadili viongozi hao ni kuhusu hatua ya Marekani kujitoa katika mkataba wa nyuklia – INF.

Peskov alisema makubaliano ya kufanyika mazungumzo hayo kati ya Putin na Trump yalifikiwa wakati walipokutana mjini Paris, Ufaransa hivi majuzi.

“Wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kumalzika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia yaliyofanyika Novemba 11, mwaka huu, Rais Putin alimwambia kitu Rais Trump.

“Walikubaliana kwamba wana mambo mengi ya kujadiliana ukiwamo mkataba wa INF na wakapanga kufanya hivyo wakati wa mkutano wa G20 utakaofanyika nchini Argentina,” alisema Peskov.

Jumapili iliyopita Rais Putin na Trump walikutana mjini Paris wakati wa maadhimisho hayo ya kutimiza miaka 100 tangu vita hiyo imalizike ukiwa ni mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Kwa mara ya mwisho Putin na Trump kukutana ilikuwa ni Julai mwaka huu  mjini Helsinki na kabla ya hapo  walishakuwa na vikao vingine nje ya mkutano kama huo uliofanyika mwaka jana nchini Ujerumani na ule wa APEC uliofanyika nchini Vietnam Novemba mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles