25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Hakimu akubali kesi ya Kaburu kusikilizwa mfululizo

NA KULWA MZEE, DAR EA SALAAM

MAKAMU wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange maarufu Kaburu ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza mfululizo kesi inayomkabili yeye na waliokuwa viongozi wenzake wawili sababu ya kuchukua muda mrefu.

Kaburu na wenzake wanakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na kughushi, kesi yao ilikwama jana kuendelea mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Kesi hiyo ilikwama kuendelea na ushahidi baada ya upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa kielelezo mahakamani.

Kielelezo kilichokataliwa kilitolewa na shahidi wa kwanza, Boaz Mbupila ambaye ni msimamizi wa Benki ya CRDB anayeangalia kama benki inakidhi taratibu za kibenki.

Boaz alitoa kielelezo cha taarifa ya benki ya fedha na taarifa nyingine ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Vielelezo hivyo vilipingwa kwa sababu upande wa Jamhuri hawakuonyesha msingi kabla ya kuomba kutoa vielelezo hivyo.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili aliahirisha kesi na kupanga Novemba 26 kwa ajili ya kutolew uamuzi.

Hata hivyo Hakimu huyo amekubali maombi ya Kaburu na kuipanga kesi hiyo kusikilizwa mfululizo kuanza Novemba 26, Desemba 4 na 5 mwaka huu.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba,  Evans Aveva,  Makamu wake,  Geofrey Nyange na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles