29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaka aipa tano World Vision uanzishwaji kiwanda cha sabuni

Derrick Milton, Simiyu



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amelipongeza Shirika la World Vision nchini kwa kusaidia uanzishwaji wa kiwanda cha sabuni katika kijiji cha Kanadi Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

Mbali na kuanzisha kiwanda hicho kwenye kijiji hicho, shirika hilo limeanzisha kituo cha mafunzo endelevu kwa vijana ambapo kitatumika kwa ajili ya kufundisha vijana wa wilaya hiyo shughuli za ushonaji nguo na useremala.

Akikagua kiwanda hicho pamoja na kituo, mkuu huyo wa mkoa amesema shirika hilo, limetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuanzisha viwanda ili kifikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya, itahakikisha inakiendeleza kiwanda hicho ili kuwa kikubwa zaidi na kuwa moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya halmashauri na wananchi wa wilaya hii,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Dk. Yoshi Kasilima, amesema lengo la shirika hilo kuanzisha kiwanda hicho ni kuondoa umaskini kwa wananchi wa Wilaya hiyo hasa kijiji cha Kanadi kwa kujipatia kipato kupitia mradi huo.

“Mradi wa kiwanda na kituo umegharimu zaidi ya Sh milioni 250, ambapo zimewekwa mashine za kisasa za uzalishaji wa sabuni, majengo na mindombinu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles