32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

TLS yalaani kutekwa kwa Mo Dewji, yataka serikali kuimarisha ulinzi

Bethsheba  Wambura, Dar es Salaam



Chama cha Mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS), matukio ya utekaji yanayotokea mara kwa mara ni kielelezo kwamba usalama wa raia nchini si wa kuridhisha.

Kupitia taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Rais wake, Fatma Karume, chama hicho kimeitaka serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kuimarisha ulinzi wa raia kwa ustawi wa taifa bora lenye amani huku kikilaani kitendo cha kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu Mo Dewji.

Mo alitekwa Alhamisi wiki iliyopita katika Hoteli ya Colloseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya  mazoezi hotelini hapo.

“TLS inaungana na familia, ndugu na Watanzania wote walioguswa na kutekwa kwa  Mo na Watanzania wengine waliowahi kutekwa akiwamo Ben Saanane, Azory Gwanda na wengineo kulaani vitendo hivyo vya utekwaji.

“Tunapotafakari kutekwa na kutoweka kwa ndugu zetu hao, bila ya kuwasahau wengine tunaangalia vitendo hivi kama uvunjwaji wa haki zao msingi  na tunachukua fursa hii kuikumbusha jamii, serikali na vyombo vya usalama kuwa nchi yetu ni huru kwa mujibu wa Katiba na Ibara ya 15 inatambua umuhimu wa mwananchi kwenda kokote bila kizuizi,” amesema Fatma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles