NAIROBI, KENYA
WATU zaidi ya 50 wamefariki dunia nchini hapa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu itokayo jijini hapa kwenda Kisumu.
Vyombo vya habari vililiripoti jana kwamba ajali hiyo ilitokea katika eneo la Fort Ternan, Kaunti ya Kericho.
Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kuserereka mita 20 katika bonde.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni mwa waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano.
Awali idadi ya waliofarini ilikuwa 40, lakini polisi walielezea hofu yao juu ya vifo kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya.
“Bahati mbaya sana tumepoteza watu 51,” Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinnet alikiambia Kituo cha Redio Capital FM.
Mashuhuda walisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 11 alfajiri.
Mmoja wa mashuhuda hao aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC kwamba alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele.
Baadhi ya majeruhi wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi hospitali ya kaunti mjini Muhoroni kupatiwa matibabu.
Taarifa zaidi zilieleza kuwa miili ya baadhi ya watu waliofariki hadi mapema jana ilikuwa bado imekwama ndani ya mabaki ya