25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo IPTL waendelea kusota rumande

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM


UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi na James  Rugemarila, umetakiwa kukamilisha upelelezi ili hatma ya kesi hiyo ijulikane.

Jamhuri ilitakiwa kufanya hivyo jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa. Jamuhuri ilisema upelelezi haujakamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alisema kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba  upelelezi haujakamilika.

Wakili wa Rugemarila, Didas Respicius alieleza   kuwa sera ya mahakama ni mashauri yasikilizwe na kutolewa uamuzi kwa wakati.

Alidai wanashangaa kila kesi inapokuja upande wa mashtaka unaomba tarehe ya kuitaja kesi kwa zaidi ya mwaka sasa, wakati washtakiwa wanateseka mahabusu.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Kishenyi alidai  wataendelea na upelelezi ili pande zote mbili zipate haki sawa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Shaidi aliutaka upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi  hatma ya kesi ijulikane.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya Dola za Marekani  22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles