28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

VIONGOZI WAMSIFU KOFI ANNAN


ACCRA, GHANA

Viongozi mbalimbali duniani waliohudhuria mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan yaliyofanyika mjini Accra nchini Ghana juzi, walimmwagia sifa kemkemu na kubainisha kuwa ulimwengu umempoteza mtu muhimu sana.

Katika mazishi hayo mjane wake, Nane Maria Annan, aliwaongoza mamia ya waombolezaji, wakiwemo viongozi wa sasa wa dunia na wa zamani waliohudhuria ibada hiyo ya mazishi ya kitaifa.

Rais wa Ghana, Nana Akufo Ado, alimtaja Annan kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri kabisa wa zama hizi.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alimsifu marehemu akisema alikuwa kiongozi wa kipekee duniani aliyekuwa mwenye heshima, jasiri na mtu aliyekuwa mwadilifu na aliyejitolea katika kazi yake.

Annan aliyeongoza Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1997 hadi 2006 na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2001, alifariki dunia nchini Uswisi Agosti 18 mwaka huu, akiwa na umri wa miaka 80.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles