25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAJASIRIAMALI WAMEBEBA UCHUMI TANZANIA

Katibu wa Utawala wa Taasisi ya Ubunifu wa Biashara ya Kilimo, Sandra Nassoro, akitoa maelezo namna matumizi ya bidhaa wanazotengeza hivi karibuni.

Na Bakari Kimwanga – DAR ES SALAAM


TANZANIA ni moja ya nchi barani Afrika ambazo uchumi unakuwa kwa kasi.

Tangu mwaka mwaka 2017 kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imefikia asilimia 7 na moja ya chachu ya kasi hiyo inatajwa kuwa ni biashara ndogondogo ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na wanawake.

Takwimu za usawa wa kijinsia katika ajira zinaonyesha kwamba kufikia mwaka wa 2014 Watanzania milioni 2.1 walikuwa wameajiriwa katika sekta rasmi, pamoja na serikalini na sekta binafsi, kwa mujibu wa kituo cha taifa cha takwimu nchini humo.

Hata hivyo takwimu rasmi za serikali zinaonyesha pia kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wanawake walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 yaani milioni 13.9 wanajishughulisha na shughuli zisizo rasmi yaani biashara ndogondogo na kilimo.

Hatua hii maana yake ni kwamba ni asilimia 0.75 tu ya wanawake walioko katika umri wa kufanya kazi ndio wapo katika sekta rasmi.

Kwa maneno mengine, idadi kubwa ya wanawake walioko katika umri wa kufanya kazi nchini Tanzania ni wajasiriamali.

Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanawake wenye ujasiri wa kubuni na kuendesha biashara, kasi ya ukuaji wa mitaji yao bado ni finyu.

Chanzo kikuu cha mitaji karibuni duniani kote ni mikopo rasmi ya kibiashara. Hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa wanawake wengi wajasiriamali kutoka nchi zinazoinukia ikiwemo Tanzania hawana mikopo kutoka benki na taasisi rasmi za kifedha.

Kwa miaka mingi, dhana iliyoaminika ni kuwa wanawake wengi hawapati mikopo sababu fedha hazitoshi, lakini takwimu zinapingana na dhana hiyo.

Utafiti uliochapishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2014 unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maombi ya mikopo ilitengwa kwa ajili ya wajasiriamali wanawake na asilimia 90 iliiva kwa ajili ya kutolewa.

Hata hivyo asilimia 18 ya wanawake wajasiriamali ambao waliomba mikopo benki na asilimia 28 waliomba mikopo katika taasisi nyenginezo za kifedha.

Moja ya wataalamu waliondaa utafiti huo Vanessa Naegels hivi karibuni ameandika katika jarida la The Conversation kuwa, utayari wa wanawake kuomba mikopo unaathiriwa na mambo makuu mawili, dhana hasi juu ya mikopo rasmi ya kifedha na kukatishwa tamaa.

Ni kwamba ujasiriamali utaendelea kuwepo kwani kila shughuli itakayofanyika itahitaji mchanganyiko wa wawekezaji ili kufanikisha ukuaji wake.

Uchumi wa viwanda unaweka mkazo wa uzalishaji viwandani katika viwanda mbalimbali  na kwa viwango tofauti na uwezo unaotegemea uwekezaji wa mtu, kampuni na tasisi yenyewe.

Hivi karibuni Mratibu wa Huduma za Biashara wa Mradi wa Engine Zanzibar, Abasi Makame Muhamed, amesema wananchi wengi wamekuwa na mwamko wa kufanya biashara na kuzizalisha lakini wanashindwa kujua namna ya kuzitafutia masoko.

Anasema wafanyabiashara hususani wajasiriamali wamekuwa wanashindwa kutafuta mbinu za kupata mafunzo ya kuweza kuimarisha biashara zao jamba ambalo linachangia kudumaza maendeleo ya biashara zao.

Anasema wakati umefika kwa wafanyabishara hao kuondokana na utegemezi wa kupatiwa mafunzo kutoka serikalini badala yake wawe na utaratibu wa kutafuta na kununua mafunzo kutoka kwenye taasisi binafsi ili kujua namna ya kuuza biashara zao na jinsi ya kupata mikopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles