27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NIDA KUTOA VITAMBULISHO KWA WALEMAVU KINONDONI

Na Elizabeth Joachim, Dar es Salaam



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amezindua zoezi la uandikishwaji  wa Vitambulisho vya Taifa kwa watu wenye ulemavu ili kuwarahisishia kupata huduma hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Septemba 12, katika viwanja vya Shule ya msingi Makurumla iliyopo  kata ya Ndugumbi wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es salaam, amesema mpaka sasa asilimia 60 ya wananchi wameshaandikishwa ili kupata vitambulisho vya taifa.

“Kumekuwa na changamoto kwa watu wenye ulemavu katika kujiandikisha usajili wa vitambulisho vya Taifa hasa  pale unapokuta walemavu wamekaa sehemu moja na watu wasio na ulemavu,sasa ni wakati wao kupata urahisi wa zoezi hili kwa izi siku tatu,”amesema Chongolo.

Amesema kujisajili kwenye Vitambulisho vya Taifa kwa walemavu kutasaidia kujua aina ya ulemavu walionao na kujua sehemu wanayotokea na hii itarahisisha kuwapata.

Kwa upande wake Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),  Wilaya ya Kinondoni,Dicksoni Mbanga amesema wanategemea kuwafikia Walemavu wengi katika wilaya ya  kinondoni na zoezi hilo litafanyikia katika vituo vilivyopo wilayani hapo.

“Wananchi wenye ulemavu wameshapewa fomu za kujisajili kupitia vyama vyao japo bado hatujajua idadi kamili ya watu tutakaowasajili kwenye zoezi hili lakini kadri siku zinavoenda tutajua wangapi watajisajili baada ya kurudisha fomu” amesema Mbanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles