25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

DK.  KALEMANI AZINDUA MRADI WA REA WA SH. BILIONI 39 

  Na WALTER MGULUCHUMA,KATAVI



Waziri wa Nishati, Dk. Medadi Kalemani amezindua mradi wa  REA, awamu ya tatu mkoani Katavi ambao utekelezaji wake utatumia ziaidi ya Sh bilioni 39.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, alisema REA awamu ya  tatu katika mkoa huo itafaidisha vijiji 116 ambavyo havina huduma  ya umeme.

Alisema umeme huo  utasambazwa katika vijiji vyote  na Kampuni ya China Railway  Constration Company Limited iliyopewa mkataba wa miezi 24 kukamilisha mradi huo.

Dk. Kalemani alimwagiza   mkandarasi wa mradi huo  kusambaza umeme maeneo yote ya taasisi za serikali.

Pia alimtaka kusambaza umeme  kaya kwa kaya bila kubagua nyumba hata kama ni ya nyasi.

Alisema  mradi huo unatarajia kuwafikia wananchi 10,000 na utakuwa endelevu .

Aliwaonya watu wenye tabia ya kuharibu miundombinu ya umeme kaacha tabia hiyo kwa sababu inasababisha hasara.

Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi, Amos Makalla, alisema mkoa  huo bado unao mahitaji ya   umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles