25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WABUNGE WANAWAKE WAKUSANYA SH BIL 2.5 UJENZI WA VYOO



Na ANDREW MSECHU

CHAMA cha Wabunge Wanawake wa Bunge la Tanzania, wamefanikiwa kukusanya Sh milioni 800 kwenye harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo cha mfano kitakachojengwa katika majimbo yote nchini.

Fedha hizo zimekusanywa kupoitia harambee iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi kwenye alikuwa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda, lengo likiwa ni kufiisha Sh bilioni 3.5.

Kwa makusanyo hayo yanafanya wabunge wanawake kufikisha Sh bilioni 2.5, baada ya kukusanya fedha nyingine kupitia harambee ya awali iliyofanyika mjini Dodoma,i Juni, mwaka huu.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo, Makinda ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi alisema uamuzi ambao umefanywa na wabunge wanawake na kuungwa mkono na wabunge wanaume katika kufanikisha fedha zinapatikana ni wa kihistoria.

  “Tunatambua changamoto wanazopata wanafunzi hasa kwa mtoto wa kike kutokana na maumbile yake, hivyo ujenzi wa choo cha mfano katika kila jimbo utasaidia kuwafanya wanafunzi hao kufurahia mazingira yatakayokuwamo wakiwa shuleni,” alisema.

Alisema wanafahamu matatizo wanayoyapata watoto wa kike wakiwa shuleni hasa wanapofkia hatua ya kuvunja ungo, kutokana na mabadiliko yanayoanza kutokea na wanapokuwa kwenye tarehe zao ambapo wengine hulazimika kutokwenda shule kutokana na mabadiliko yao ya kimwili, hivyo ujenzi wa vyoo hivyo utawaondolea mabinti wasiwasi.

Aliwataka Watanzania kokote walipo kuchangia ujenzi wa choo hicho kwani lengo na kumuondolea adha mwanafunzi na hasa mwanafunzi wa kike.

Makinda alisema hatua ya wabunge hao kuamua kuchangisha ni ya thamani kwa kuwa italeta ukombozi kwa watoto wa kike kwa kuwawekeza mazingira rafiki ya kuwapa uhuru wa kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema wanatambua umuhimu wa kuunga mkono jitihada za wabunge wanawake katika kuhakikisha wanatimiza lengo la ujenzi huo wa vyoo vya mfano katika kila jimbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles