26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WADOGO WA MKONGE WAILALAMIKIA KAMPUNI YA KATANI

|Susan Uhinga, Tanga



Wakulima wadogo zaidi ya 100  wa  zao la  mkonge mkoani Tanga, wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuanzisha soko huria kwa ajili ya ununuzi wa zao hilo ili malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha tani 100,000 kwa mwaka yafikiwe.

Aidha, wakulima hao wameilalamikia Kampuni ya Katani Ltd. kwamba inachukuwa asilimia 54 na kumuachia mkulima asilimia 46 jambo walilodai ni unyonyaji unaofanywa na kampuni hiyo.

Wakulima hao wametoa malalamiko yao walipokutana kwa ajili ya kujadili changamoto zinazoendelea kujitokeza katika kilimo cha zao la mkonge leo Ijumaa.

Katika kikao hicho pia wakulima hao walijadili suala la bei na namna ambavyo sera  iliyowekwa na serikali inayoelekeza kuwa kila mwaka mkonge uzalishwe tani 100,000 na kwamba sera hiyo haisimamiwi ipasavyo.

“Tunaona hata utekelezaji wa hii sera iliyowekwa na serikali ya kuzalisha tani hizo  kila mwaka haupo kwa kuwa hali ni tofauti kabisa,” amesema mmoja wa kulima hao Greyson Nyari.

Kwa upande wake Ofisa Miradi wa Kampuni ya katani Ltd, Ally Mohamed amesema kwa hivi sasa hawawezi kujibu tuhuma hizo na kwamba shauri hilo linafanyiwa kazi na waziri wenye dhamana.

“Hatuwezi kujibu hapa baadhi ya changamoto za wakulima kwa sababu shauri hilo tayari lipo kwa Waziri wa Kilimo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles