LUANDA, ANGOLA
MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini hapa, Jonas Savimbi, utafukuliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ili apewe mazishi ya heshima.
Savimbi aliuawa na vikosi vya Serikali Februari 22, 2002 na kuzikwa siku iliyofuatia kwenye mkoa ulio mashariki wa Moxico.
Wiki sita baada ya kifo chake, Unita walisaini makubaliano ya amani na Serikali kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka 27.
Kiongozi wa sasa wa Unita, Isaias Samakuva, alitangaza kuwa mwili wa Savimbi utafukuliwa baada ya kukutana na Rais Joao Lourenco kwenye mji mkuu Luanda juzi.
Mapema mwezi huu, Samakuwa aliilaumu Serikali kwa kumnyima Savimbi maziko ya heshima.