26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI: UCHAGUZI WA MARUDIO TANZANIA ULIGUBIKWA NA VURUGU

Mwandishi Wetu, Dar es Salaa

Marekani imesema, uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika katika maeneo mbalimbali nchini, uligubikwa na vurugu na ukiukwaji wa sheria.

Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini, imesema nchi hiyo imesikitishwa na uendeshaji wa uchaguzi katika baadhi ya maeneo ambapo taarifa za kuaminika zinaonyesha kuwa chaguzi hizo ziligubikwa na vurugu zilizohusiana na uchaguzi.

Imesema ukiukwaji wa sheria za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kukataa kwa baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwasajili wagombea kutoka vyama vya upinzani, vitisho vya polisi dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani.

“Watu kukamatwa kiholela bila kuwepo vibali vya ukamataji na kukandamizwa kwa uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni katika kipindi chote kuelekea chaguzi hizo.

“Mambo haya yanakwaza haki ambazo Katiba ya Tanzania imewapa raia wake na kuhatarisha amani, utulivu na usalama nchini na katika eneo lote la kanda,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

SOMA ZAIDI… http://mtanzania.co.tz/57248-2/

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles