|Mwandishi Wetu, Kigoma
Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma, mkoani Kigoma, kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la michikichi nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hayo leo Jumapili Julai 29, mkoani hapa akiwa katika ziara yake ambapo pamoja na mambo mengine ameuagiza uongozi wa gereza hilo kuongeza nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi.
“Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo, kila mwananchi lazima awe na shamba la michikichi,” amesema.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=ipzj62ON05w[/embedyt]
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, Sabas Matolo kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwamo matrekta na vifaa vya kuvunia ili kuongeza uzalishaji wa mafuta.
Awali, Mkuu wa gereza hilo, Majuto Masila alisema ili kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta uweze kuwa na tija, wanahitaji wafungwa wasiopungua 300 wawepo kila siku gerezani hapo ili kumudu shughuli za shamba hilo na lwamba kwa sasa kuna wafungwa 112.