26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA ZUMA YAAHIRISHWA

President Jacob Zuma gestures during his question and answer session in Parliament in Cape Town, South Africa, September 13, 2016. REUTERS/Mike Hutchings

PIETERMARITZBURG, AFRIKA KUSINI

JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini, jana ameahirisha kesi ya ulaji wa rushwa inayomkabili rais mstaafu, Jacob Zuma, hadi Novemba 30, mwaka huu.

Zuma, ambaye alihudhuria kesi hiyo akiwa amevalia suti nyeusi na tai nyekundu, akabiliwa na makosa 16 ya udanganyifu, utakatishaji wa fedha unaohusisha tenda ya ununuzi wa silaha zenye thamani ya dola bilioni 2.5 zilizonunuliwa kwaajili ya jeshi la nchi hiyo.

Kesi hiyo, ambayo inachukuliwa kama mfano wa viongozi wa Afrika, Zuma anakabiliwa na mashtaka hayo kutokana na vitendo vyake alipokuwa madarakani, lakini amekanusha kufanya jinai yoyote.

Wakili wa Zuma, Mike Hellens, akiwa mahakamani hapo, alimuomba Jaji anayesikiliza kesi hiyo kuiruhusu timu ya mawakili wanaomtetea Zuma kufungua shauri la kupinga tuhuma hizo dhidi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali.

Jaji Mjabuliseni Madondo, ambaye anasikiliza keshi hiyo, alijibu maombi ya upande wa utetezi kuwa mawakili hao walipaswa kuandaa muda na kuwasilisha maombi yao.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 30, mwaka huu, ambapo upande wa mashtaka utawasilisha ushahidi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles