MSANII chipukizi katika muziki wa Bongo Fleva, Bhoke Joseph (Honeyb), ameibuka na wimbo wa ‘Naipenda Tanzania’ unaoelezea uzuri wa Tanzania.
Katika wimbo huo uliorekodiwa katika studio ya Steam iliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam chini ya prodyuza Master, inaelezea mambo mbalimbali yaliyoiwezesha Tanzania kuwa hapa ilipo.
Wimbo huo pia umewaelezea viongozi wote walioongoza nchi hii hadi sasa huku ikiwataka watakaokuja waendeleze Watanzania na amani yao.
“Nimeimba wimbo huo kwa sababu ya kuipenda nchi yangu na kuwakumbusha viongozi wajao waendeleze amani iliyopo ambayo ndiyo inayotuunganisha pamoja na kutufanya kuwa taifa la kuigwa na nchi nyingine katika amani,’’ alieleza Honeyb.