26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU KESI YA VIGOGO CHADEMA AGOMA KUJITOA, ASEMA HAJAWAHI KUKATALIWA KWA SABABU ZA AJABU AJABU

                                                                |Kulwa Mzee, Dar es Salaam                                                 

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe amegoma kujitoa.

Hakimu Mashauri ametoa uamuzi huo leo Jumanne Julai 10,  baada ya kuombwa na washtakiwa hao kujitoa wakidai hawana imani naye.

“Ilitolewa sababu kwamba kwa mwonekano wa hakimu hawezi kutenda haki, niko katika benchi hili kwa miaka 22 sasa sijawahi kuombwa kujitoa kwa sababu za ajabu ajabu kama hizi, sababu hiyo sikuitilia maanani.

“Nimepitia sababu zote za kutaka nijitoe lakini maombi hayo hayana mashiko ya kutosha kunikataa,” amesema Hakimu Mashauri.

Aidha, Hakimu Mashauri amesema aliziona sababu zote zaidi ya 10 hazina msingi ikiwamo kwamba anapendelea upande wa Jamhuri na kwamba ana nia ovu ya kutaka kuzika haki.

Washtakiwa katika kesi hiyo wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali, kufanya uchochezi wakiwa katika mkutano wa kampeni za Jimbo la Kinondoni, Viwanja vya Buibui Februari mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles