29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

WANANCHI WAPINGA KUHAMISHWA MAKABURI

Na ERICK MUGISHA (DSJ) – DAR ES SALAAM


WANANCHI wa Mtaa wa Makangarawe Wilaya ya Temeke,  Dar es Salaam wamepinga kuhamishwa   makaburi  wanayotumia kuzikia kupisha ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Wakizungumza na MTANZANIA jana baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema eneo hilo   awali lilikuwa linamikiwa na mtu binafsi aliyeamua kulitoa kwa wananchi litumike kuzikia.

Kwa mujibu wa wananchi hao,  hadi sasa eneo hilo lina zaidi ya makaburi 300 hivyo wanapinga uamuzi huo wa kutaka kuyahamiasha.

Mkazi wa eneo hilo, Mohamedi Matope, alisema yeye na wenzake watano walikwenda kwa Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam, Paul Makonda,m kufikisha kilio chao lakini walijikuta wakigonga mwamba baada ya kuambiwa kiongozi huyo yupo kwenye vikao na kutakiwa kurejea baada ya wiki mbili.

Naye Abdalah Katuni alidai kuwa mwenyekiti wa mtaa amekuwa akiwaendesha kwa mabavu ambako wao wanaopinga  wamekuwa wakipokea vitisho kutokana na msimamo wao wa kuhamishwa  makaburi hayo.

MTANZANIA ilifika  katika ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Makangarawe na kuzungumza na na mwenyekiti wa mtaa huo, Denis Moyo.

Alisema suala la kuhamishwa   makaburi hayo linatokana na uamuzi wa Manispaa ya Temeke ambayo imedhamiria kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja wa mpira, soko  a na hospitali ya kisasa katika eneo hilo.

“Ninachofahamu hapa kuna mradi mkubwa na Benki ya Dunia ambayo ipo tayari kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake. Jambo lolote linapokuja ni lazima watakuwapo wanaopinga na wanaohitaji kuwapo kwa maendeleo ya eneo letu.

“…hiki ndicho ninachofamu ila kama unataka maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ambaye  ofisi yake inasimamia suala hili,” alisema Moyo.

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke  kupata ufafanuzi   kuhusu suala hilo hakupatikana na MTANZANIA inaendelea na juhudi za kumtafuta  kupata ufafanuzi wa kina wa suala hilo ikiwamo kuhamishwa  makaburi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles