Na Mwandishi wetu     |   Â
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali inafuatilia kwa karibu taasisi za kiraia na kwamba zikibainika zinafanya kazi kinyume na majukumu yake, zitachukuliwa hatua kali za kisheria.
Ametoa kauli hiyo Bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Longido, Dk. Stephen Kiruswa ambaye alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuzichukulia hatua taasisi za kiraia ambazo zinafanya kazi za siasa.
Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema serikali inafuatilia kwa karibu kazi zinazofanywa na taasisi za kiraia na kwamba tayari zipo zilizopewa tahadha kwa kufanya kazi kinyume na majukumu yao.
“Ikibainika hazitimizi wajibu na kufanya kazi nje na majukumu yao na kuleta mtafaruku, hatutasita kuzichukulia hatua kali za kisheria,” amesema.