25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kipindupindu chatua Dar

NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

UGONJWA wa kipindupindu umelipuka tena Dar es Salaam na kusababisha watu kadhaa kulazwa katika hospitali mbalimbali.

Wagonjwa hao wamelazwa katika hospitali za Sinza  Palestina na Mwananyamala.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani, alisema wagonjwa waliothibitika kuwa na kipindupindu na kulazwa hospitalini hapo ni wawili.

Alisema wagonjwa hao ambao ni mwanamke na mwanaume wanatoka   Tandale na Mwananyamala.

Taarifa nyingine zilisema wagonjwa kadhaa wa kipindupindu wamelazwa katika Hospitali ya Palestina Sinza.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo hakuwa tayari kutaja idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.

“Sisi tunakusanya taarifa zote na kuziwasilisha wilayani…nenda huko watakupatia,” alisema mganga huyo.

Mara ya mwisho ugonjwa huo ulilipuka  Dar es Salaam mwaka 2010 ambako watu 17 walilazwa wakitokea Manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala.

Mara ya mwisho ugonjwa huo ulilipuka Dar es Salaam mwaka 2010 ambako watu 17 walilazwa wakitokea Manispaa
za Temeke, Kinondoni na Ilala.

kutokana na ugonjwa huo wananchi wametakiwa kuzingatia suala la usafi pamoja na kufuata kanuni za afya ili kuepuka magonjwa ya mlipuko,ikiwemo kipindupindu.

Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es salaam. Judithi Kahama,imeonyesha kuwa kulipuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu katika jiji la Dar es salaam hivi karibuni kunatokana na baadhi ya wananchi kushindwa kufuata kanuni za afya.

Kanuni hizo za usafi ni pamoja na kuchemsha maji ya kunywa,kunawa mikono na sabuni,kuosha matunda na kula
vyakula vya moto.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa,elimu ya afya bado inaendelea kutolewa kwa wananchi ikiwa ni juhudi za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo pamoja na wananchi kupata elimu ya kutosha juu ya
kujikinga.

Ugonjwa wa Kipindupindu umeripotiwa kulipuka Jijini Dar es salaam na mpaka sasa kuna taarifa ya wagonjwa 11 kutoka katika Manispaa tofauti za Jiji la Dar es salaam wameripotiwa kulazwa hospitalini kwa kuugua ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles