25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

VYURA 9,000 WAREJESHWA MAENEO YA ASILI


Na Mwandishi Wetu-Morogoro  |

ZAIDI ya vyura wa Kihansi 9,873, wamesharudishwa katika maeneo yao ya asili yanayopatikana katika safu za Milima Udzungwa mkoani Morogoro, tangu walipoanza kurudishwa kidogo kidogo mwaka 2012.

Vyura hao wanaopatikana Tanzania pekee, wanatokana na idadi ya vyura 500 waliopelekwa Marekani kwa ajili ya kuhifadhiwa katika maabara maalumu mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kuwepo hatari ya kupotea.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Morogoro, Mtafiti wa Viumbe Pori kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Charles Msuya, alisema historia ya vyura wa Kihansi ni kubwa na namna ya kuwarudisha katika makazi yao pamoja na kutafiti tabia na maadui zao si ndogo, hivyo amewataka wadau wa mazingira na viumbe hao kutumia nafasi na uwezo wao kuhakikisha vyura wanabaki salama.

“Leo tumerudisha vyura katika eneo lao la asili, hawa ni mchanganyiko wa vyura kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na maabara ya Tawiri (Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania) iliyopo hapa hapa Kihansi, tangu tulipoanza huu utaratibu mwaka 2012 hadi sasa tumesharudisha zaidi ya vyura 9,873.

“Tuliwagundua vyura wa Kihansi mwanzoni mwa miaka ya 1990, hii ni aina ya kipekee ya vyura duniani ambao mayai yao wanayahifadhi tumboni na kuzaa kama mamalia badala ya kutoa mayai, kuanzia miaka ya katikati ya 1990, Tanesco walianzisha mradi wa kufua umeme wa Lower Kihansi kwa kutumia maji yaliyokuwa yakitiririka katika Bonde la Kihansi, ndipo vyura walipoanza kufa,” alisema Dk. Msuya.

Alibainisha kuwa baada ya kuona hali ni mbaya wakatafuta namna ya kuwaokoa na kufanikiwa kupeleka vyura 500 nchini Marekani, ili wakati wakiendelea na mambo mengine wawe na uhakika walau viumbe hao adimu duniani wapo salama kwenye maabara.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles