25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO YABADILI MFUMO WA MALIPO YA UMEME


Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM   |

WATEJA wa Umeme wanaolipa baada ya kutumia (Post paid) sasa wametatakiwa kulipia ankara zao katika taasisi za fedha na si Tanesco.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Leyla Muhaji alisema mfumo huo wa malipo umeanza kutumika rasmi jana.

Alisema katika mfumo huo, mteja hahitaji kwenda kupanga foleni Tanesco bali atalipia kwa njia za benki na mitandao ya simu.

“Wanapopata ankara zao watalipia kupitia Mpesa, Tigopesa, Hallopesa na benki za NMB, CRDB, NBC na mawakala wa benki hizo,” alisema Leyla.

Alisema tayari wataalamu kutoka Tanesco wamekwenda mikoa yote nchini kutoa elimu kuhusu mfumo huo mpya.

“Mfumo huo uko kkwa mujibu wa sheria na unazitaka taasisi za serikali kutumia mfumo wa malipo ya elektroniki wa serikali hivyo nasi Tanesco tumejiunga,” alisema Leyla.

Alisema mfumo huo ni salama kwa pande zote yaani Tanesco na mteja.

“Mfumo huu uko wazi kwa mteja kujua alicholipa na Tanesco wanaona malipo yaliyofanyika,” alisema Leyla.

Alisema wako katika mchakato wa kuwaingiza wateja hao katika malipo ya kabla (pre paid) ili kwenda sambamba na teknolojia ya kisasa.

“Wateja wetu wa malipo ya kabla tayari wameingia katika mfumo huu na sasa tunahitaji kuwaingiza wateja wa malipo ya baada ambao ni wachache,” alisema Leyla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles