BEIJING, CHINA
KITUO cha habari cha CNBC nchini Marekani kimeripoti kuwa China imeweka mifumo ya makombora ya kushambulia meli na kudungua ndege kwenye visiwa vitatu vilivyoko Bahari ya China Kusini.
Visiwa hivyo umiliki wake umekuwa ukigombaniwa kati ya China na nchi jirani.
Ikiwa taarifa hizo zitathibitihwa, itakuwa mara ya kwanza kwa China kuweka makombora katika visiwa hivyo ambayo Vietnam na Taiwan zinadai ni himaya yake.
CNBC imenukuu duru za kijasusi nchini Marekani, zikisema mfumo huo wa makombora uliwekwa katika visiwa hivyo siku 30 zilizopita.
Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi ya China haijatoa tamko lolote kuhusu makombora hayo, lakini imesisitiza zana zozote za kijeshi ilizoweka katika visiwa hivyo ni kwa ajili ya kujilinda.