Na Mwandishi wetu    | Â
Serikali imeyaagiza makampuni makubwa ya uchimbaji wa madini nchini kutoa maelezo ya taarifa ya fedha zilizotumika au kutengwa kwa ajili ya uwajibikaji na ufadhili wa miradi mbalimbali kwa jamii.
Agizo hilo limetolewa bungeni leo mjini Dodoma na Waziri wa Madini, Angela Kairuki wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Vicky Kamata (CCM), aliyetaka kujua makampuni makubwa ya uchimbaji wa madini ikiwamo Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) yametoa fedha kiasi gani kufadhili miradi ya kijamii.
Kairuki amesema GGM imetumia kiasi cha Sh bilioni 14.45 kwa mwaka 2017 lakini ameagiza itoe maelezo namna fedha hizo zilivyotumika.