ADDIS ABABA, ETHIOPIA
WAZIRI Mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed, jana alitangaza baraza lake la mawaziri linalojumuisha waziri wa zamani wa madini ambaye sasa anakuwa wa ulinzi.
Aidha amewabakisha mawaziri wa fedha na mambo ya nje waliokuwa katika Serikali ya mtangulizi wake.
Ahmed aliyeteuliwa mwezi uliopita na muungano unaotawala nchini Ethiopia, ambaye mapema mwezi huu aliapishwa kushika uwaziri mkuu, alitangaza uteuzi huo kupitia televisheni ya taifa.
Ofisa huyo wa zamani wa jeshi alitoa wito kwa Bunge kuidhinisha mabadiliko aliyoyafanya yanayowahusu mawaziri sita na uteuzi mpya wa mawaziri wengine 10.