29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

ZEC yawapiga msasa vijana Z’bar

Na Is-haka Omar, Zanzibar
TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewataka vijana kutambua haki yao ya kushiriki kwa ukamilifu katika Uchaguzi Mkuu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanalinda amani ya nchi.
Rai hiyo ilitolewa jana na Kamishna wa ZEC, Ayoub Bakar Hamad, katika Kongamano la Vijana na Uchaguzi mjini Unguja.
Alisema utafiti mbalimbali unaonyesha kuwa katika uchaguzi uliopita kundi la vijana limekuwa likitumiwa wanasiasa kuvuruga uchaguzi na kukiuka taratibu zilizowekwa na tume hiyo.
Alisema ZEC inakusudia kuhakikisha kundi hilo linakuwa sehemu muhimu ya kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unafanyika kwa amani na utulivu.
“Vijana mmekuwa mkitumikishwa sana na wanasiasa katika uchaguzi lakini hao mnaowatumikia wakishapata uongozi hawakukumbuki tena wakati mmeshapoteza haki zetu kwa maendeleo ya baadae jambo ambalo kwa mwaka huu tumekusudia kulimaliza ama kulipunguza.

“Mbali na hilo baadhi ya viongozi wa siasa wamekuwa wakisikika wakihamasisha vurugu kupitia majukwaa ya siasa tena wakisema wanayo hazina ya vijana ambao watawatumia kufanikisha masilahi yao na hao ndiyo wanaokuwa wakitumika kupinga hata matokeo ya uchaguzi na kuingiza nchi katika machafuko,”alisema Ayoub.
Naye Mkurugenzi wa ZEC, Salum Kassim Ali, alisema lengo la kongamamo hilo ni kuhakikisha vijana wanakuwa wadau muhimu wa kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uweze kuwa wa amani na utulivu.
Alisema licha ya kuwapo baadhi ya changamoto za usalama katika uchaguzi uliopita, bado ZEC kwa kushirikiana na wadau wengine, wana fursa ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu kumaliza changamoto hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles