Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM |
RIPOTI ya makadirio ya idadi ya watu nchini kuanzia mwaka 2013 hadi 2035, inaonyesha nusu ya watu nchini ni wategemezi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), asilimia 50 ya watu wote nchini ni watoto walio chini ya miaka 18.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha asilimia 44 ya watu wote nchini wana umri chini ya miaka 15.
Akizungumza jana wakati wa kuwasilisha matokeo ya makisio hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa, alisema idadi ya watu nchini imefikia milioni 54.2 – Tanzania Bara milioni 52.6 na Zanzibar milioni 1.6.
Alisema kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6, hivyo ifikapo 2022 kutakuwa na watu milioni 61.2.
“Idadi ya watu nchini inaendelea kukua na hili si kosa, katika nchi yoyote inayoendelea duniani rasilimali watu ni kitu cha kwanza. Kama huna watu huwezi kufanya kazi na maendeleo yoyote tunayotafuta ni kwa ajili ya watu,” alisema Dk. Chuwa.
Alisema makadirio hayo yamezingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 na viashiria vingine vya uzazi na vifo vinavyotokana na tafiti zilizofanyika baada ya sensa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kasi kubwa ya ongezeko la watu inasababishwa na ….
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.