Na ELIYA MBONEA-ARUSHA |
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Tanzania ina dalili za kuvunja mfumo wa vyama vingi kutokana na uhusiano kati ya vyama vya siasa kuwa wa uadui unaohusisha kutesa watu na kuua kuliko ushindani wa hoja za kisiasa.
Kutokana na kuibuka kwa matukio hayo, alisema chama hicho kinapendekeza uitishwe mkutano wa kitaifa wa maridhiano ya kisiasa na changamoto za uendeshaji siasa hapa nchini zitajadiliwa na kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi.
Akizungumza mjini hapa jana alipokuwa akifafanua ziara ya kutembelea kata zilizochagua madiwani wa chama chao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema ubinywaji wa haki za siasa kwa vyama, ikiwamo kuzuia mikutano ya hadhara, kumejenga hisia kuwa watawala hawataki mfumo wa vyama vingi.
“Kufanya siasa nchini kwa sasa imekuwa ni jambo la hatari kiusalama. Hii ni dalili mbaya, usalama wa wananchi umeendelea kuwa mbaya siku hadi siku,” alisema Zitto na kuongeza:
“Mauaji ya raia yanaendelea, bahati mbaya yana sura zote za kisiasa. Utamaduni wa mauaji unaanza kuwa wa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.