NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM |
TUKIO la kuuawa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi, limechafua hali ya hewa na kukumbusha matukio mengine yenye sura inayorandana na hilo yaliyowahi kutokea nchini.
Akwilina ambaye amezikwa juzi kijijini kwao Rombo mkoani Kilimanjaro, aliuawa Februari 16, mwaka huu kwa risasi  inayodhaniwa kufyatuliwa na polisi wakati  wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana kuelekea kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, kudai viapo vya mawakala wao.
Kuuawa kwa Akwilina na Diwani wa Chadema, Kata ya Namawala mkoani Morogoro, Godfrey Lwena wiki hii ambaye alikatwakatwa mapanga hadi kufa na watu ambao hawajajulikana limewafanya baadhi si tu kurejea matukio ya namna hiyo ya watu kupigwa risasi, kutekwa na kuteswa, bali kuanza kuona ni mambo yasiyokubalika na yasiyopaswa kuendelea kutokea tena nchini.
Uthibitisho wa hilo, ni tamko la juzi la Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), ambalo si tu limekemea matukio yenye viashiria vya ukatili na vitisho hapa nchini, bali kutaka hatua zaidi zichukuliwe kukomesha matukio hayo.
Tamko hilo la EU ambalo lilitanguliwa na lile lililotolewa na Ubalozi wa Marekani hapa nchini, yote yametaka kufanyika kwa uchunguzi ulio wazi kwa matukio ya kuuawa kwa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.