23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MADIWANI 60 WAHAMA CHADEMA


EVANS MAGEGE Na AGATHA CHARLES-DAR ES SALAAM  |  

WAKATI vuguvugu la madiwani kujiuzulu nyadhifa zao likiendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku, imebainika kwamba tangu Januari mwaka juzi hadi sasa, kata 89 ziliondokewa na madiwani wake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo vifo, kutenguliwa mahakamani na kujiuzulu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika idadi hiyo, madiwani 60 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Madiwani hao walijiuzulu na kufuata uanachama wa CCM kwa hoja kwamba wanaunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na idadi hiyo, madiwani watano wa Chadema na mmoja wa CCM walitenguliwa na mahakama katika nyadhifa zao.

Katika orodha hiyo, pia kata 23 zilibaki wazi baada ya madiwani waliokuwa wakiziongoza kufariki dunia.

Ndani ya orodha ya madiwani 23 waliofariki dunia, 19 walikuwa wa CCM, wawili Chadema, mmoja ACT-Wazalendo na mmoja CUF.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Tume ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro, ameliambia gazeti hili kwamba hadi Februari 17, mwaka huu, kata 82 zilishafanya uchaguzi kuziba nafasi zilizoachwa wazi.

Mkoa wa Arusha ndio …

kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles