26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

VANESSA HAWAZII GHARAMA YA ‘MONEY MONDAYS’

NA JESSCA NANGAWE


MWANADADA nyota wa muziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee, amesema licha ya gharama kubwa ya kuandaa albamu yake mpya lakini kubwa analoangalia ni jinsi itakavyopokelewa na mashabiki zake ndani na nje ya Tanzania.

Vanessa aliachia albamu yake mpya hivi karibuni aliyoipa jina la Moneymondays katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo alikiri kutumia zaidi ya milioni 100 katika kuikamilisha.

Alisema hajutii matumizi ya kiasi hicho kikubwa kwa kuwa lengo lake hasa ni kutoa kazi itakayomwongezea heshima kwenye muziki wake sambamba na kuhakikisha inawafikia watu wa aina zote.

“Nimetumia fedha nyingi lakini kwangu sioni tatizo lolote, niliangalia zaidi jinsi gani watu watatambua Vanessa kafika wapi katika kukua kimuziki, fedha hiyo nililipa idara zote kuanzia wasanii walioshiriki, matangazo, video, nk na bado naendelea kutoa  kwa kuwa matangazo bado yanaendelea,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles