33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

PROFESA KAIRUKI AKUMBUKWA

Na JOHANES RESPICIUS-DAR ES SALAAM


SHIRIKA la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN) limeadhimisha miaka 19 ya kumbukizi ya Muasisi wa shirika hilo, Profesa Hubert Kairuki aliyefariki dunia Februari 6, 1999.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ya Dar es Salaam jana, shirika hilo linalojumuisha Hospitali ya Kairuki, Shule ya Uuguzi Kairuki na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, ilisema katika kumbukizi imefanyika kuanzia Februari Mosi hadi sita mwaka huu itahusisha shuguli mbalimbali za kijamii.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Februari 5, mwaka huu kutakuwa na uwekwaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kusaidia watu wenye matatizo ya kupata ujauzito kwa njia ya kawaida Bunju, utoaji wa huduma za afya za msingi ikiwa ni pamoja na kupima shinikizo la damu, na kutoa ushauri.

“Pamoja utoaji wa huduma ya afya bila malipo kutafanyika uchangiaji damu litakaloshirikisha  wananchi wa maeneo ya Bunju, wanafunzi na wafanyakazi wa HKMU, Kairuki Hospitali na Shule ya Uuguzi Kairuki  kwa siku tatu mfululizo.

“Wanafunzi wa HKMU watashiriki katika shindano la kupima ujuzi juu ya mambo ya msingi katika taaluma ya afya, maswali ya ufahamu kuhusu Tanzania,  maisha ya Profesa Hubert Kairuki, Jiografia na jamii kwa ujumla.

“Taarifa hiyo ilisema kuwa katika kilele cha kumbukizi hiyo Februari 6 kutakuwa na Mhadhara wa Tisa wa Kitaaluma wa Kumbukizi ya Profesa Hubert Kairuki utakaosimamiwa na HKMU mada ikiwa ni ‘Umuhimu wake katika utoaji wa Huduma za Afya Barani Afrika’ itakayotolewa na Profesa Malise Kaisi,” ilisema taarifa hiyo.

Profesa Hubert Clemence Mwombeki Kairuki alizaliwa Juni 24, 1940  Bukoba, mkoani Kagera na kupata elimua ya Msingi katika Shule ya Msingi Kigarama na ya Kati katika shule ya Mugeza, Sekondari  akisoma Kahororo, Ilboru na Old Moshi, kati ya mwaka 1947 na 1962.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles