23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AUNGA MKONO JUHUDI ZA MENGI

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM


SERIKALI imeunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi na kumtaka aanzishe taasisi itakayoitwa jina lake ili aingie kwenye vitabu vya Serikali kama Mtanzania wa kwanza kusaidia watu wenye ulemavu.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na Dk. Mengi kwa ajili ya chakula maalum cha mchana kwa watu wenye ulemavu.

“Serikali inaunga mkono kazi nzuri iliyofanywa na Dk. Mengi kwa miaka 24, huna sababu ya kuachwa kimya, kazi hii sasa isifanywe na Mengi, tuipe jina taasisi yako ambalo Serikali imependekeza…Reginald Mengi Disabled Foundation.

“Huna sababu ya kuachwa kimya kwa uliyoyafanya, lazima uingie katika vitabu vya Serikali kama Mtanzania wa kwanza kusaidia watu wenye ulemavu, Serikali ikiunga mkono italeta misaada katika hiyo taasisi.

“Mimi naahidi kuchangia Sh milioni 10 katika taasisi, isajilini Brela haraka, fungueni akaunti, unatakiwa kuungwa mkono, hutakiwi kuachwa ukiendelea kufanya peke yako, Serikali imependekeza jina lazima tufanye kazi kwa pamoja,”alisema.

Waziri Majaliwa aliwataka wadau wengine zikiwemo kampuni kuiga mfano wa Dk. Mengi na kwamba anamuombea kwa Mungu aweze kumpa fursa ya kuendelea kusaidia watu wenye ulemavu.

Alisema Serikali imekuwa ikichukua hatua katika kuhakikisha inaondoa mtazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu sambamba na kuwahusisha kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za Serikali na hasa katika ngazi ya uamuzi.

“Miongoni mwa changamoto kwa watu wenye ulemavu ni miundombinu rafiki katika maeneo ya umma na binafsi. Mitizamo hasi, ukosefu wa mitaji, masoko na kandarasi na ukosefu wa fursa za ajira katika sekta za umma na binafsi.

Akizungumzia halfa hiyo, Dk. Mengi alisema huu ni mwaka wa 24 kwa IPP kuandaa tafrija hiyo kwa madhumuni ya kuonesha upendo na kujenga umoja kati ya watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu na kwamba huwa analisubiri kwa hamu tukio hilo.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga alieleza kusikitishwa na matokeo ya kidato cha nne kwa shule ya viziwi Njombe, Iringa ambao wote wamepata alama sifuli na kuomba Serikali itenge bajeti kwa watu wenye ulemavu na kupewa  ruzuku kwa ajili ya elimu ya juu badala ya mkopo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles