MMOJA wa wachezaji wa Tanzania, wanaoieperusha bendera ya Tanzania nchi za nje. Mroki anacheza soka la kulipwa nchini Ukraine.
Daima mchezaji huyu hawezi kukisahau kituo cha  cha kukuza vipaji cha TSA, kilichokuwa kikisimamiwa na kuongozwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwani kimeweza kumnoa vema na kumuwezesha kupata nafasi ya kukitumikia kikosi cha vijana Serengeti Boys na ile ya Ngorongoro Heroes miaka kadhaa iliyopita.
Spotikiki imeweza kufanya mahojiano na mchezaji huyu, ambaye licha ya kuishi nje ya nchi amekuwa akifuatilia kwa ukaribu masuala mbalimbali yanayolihusu taifa la Tanzania.
Siasa
Nadhani siasa yetu sio mbaya imefungua watu akili na utendaji wa watu katika majukumu yao kiserekali. Lakini upande mwingine siasa za Tanzania zimefikia pabaya watu wanauwana, wengine kutishiana maisha, jambo linalopelekea asilimia kubwa ya watu kuishi kwa mashaka, hali hii sio nzuri lazima tubadilike.
Siasa zetu zinatakiwa kujenga umoja na kuibua mijadala ya kuleta maendeleo, yanatoweza kulisogeza mbele taifa letu la Tanzania.
Elimu
Upande wa elimu sijafatilia sana ila nazani hili suala la utandawazi  limesaidia kuleta mabadiliko makubwa, kwa kiasi kikubwa mambo mengi yameweza kurahisishwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Elimu hivi sasa imekuwa rahisi, watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kusoma na kujifunza mambo mbalimbali.
Mfano mdogo ni google, imeonekana kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule na hata vyuoni, wengi wamekuwa wakijifunza na kuendelea kujifunza zaidi.
Michezo
Bado tunasuasua nazani kutokua na wazamini  wanaojitokeza kusapoti na kuwekeza. Lakini kuna mabadiliko kidogo yameonekana hivi sasa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, ikiwemo wachezaji kutoka kucheza nje. Pia vijana kupewa nafasi katika timu mbalimbali, huku klabu zikiendeela kuonyesha ushindani.
Jambo ambalo litaweza kuisaidia zaidi sekta ya michezo ni wadau na wawekezaji wengi kujitokeza kusaidia, vema ikatambulika michezo ni ajira kubwa sana duniani.
Mataifa mengi barani ulaya yamekuwa yakitajirika na kujiingizia kipato cha maendeleo kupitia michezo mbalimbali ambayo wachezaji wake wamekuwa wakishiriki.
First Eleven
David de Gea, Kyle Walker,Marcelo,Sergio Ramos, Leonardo Bonucci, N’Golo Kante, Mesut Ozil, Luka Modric, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar Jr.
Â
Â
Â
Â
Â