25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

SUMAYE, MAZRUI WAPINGA RAIS KUONGEZEWA MIAKA SABA

Na AGATHA CHARLES-DAR ES SALAAM


HOJA iliyoibuliwa ndani ya Baraza la Wawakilishi, Zanzibar  na kuonekana kuungwa mkono na Makamu wa Pili wa Rais visiwani humo, Balozi Seif Ali Idd, ya kutaka rais aongezewe muda wa kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba, imepingwa vikali na wanasiasa wa upinzani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa simu jana, wanasiasa hao walisema hoja hiyo haina mashiko kwa kuwa miaka mitano iliyopo kikatiba inatosha kufanya maendeleo kwa mtu au chama kilichopo madarakani.

Miongoni mwa wanaoipinga hoja hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na wanasiasa na viongozi wa CUF, Ismail Jussa na Nassor Ahmed Mazrui ambao wameifafanisha hoja hiyo na jambo baya, linalotoa taswira ya kuwako kwa hofu.

SUMAYE

Akizungumzia hoja hiyo, Sumaye alisema ni suala baya kwani wanaozungumzia kuongeza muda wametanguliza masilahi yao binafsi na yale ya vyama vyao.

“Ni suala baya kabisa, kimsingi watu wanaozungumzia miaka saba ni wale ambao wanatafuta namna ya kutawala kwa muda mrefu kwa sababu za masilahi binafsi au ya chama. Miaka mitano ndiyo Katiba yetu inavyosema na ndio muda mwafaka kuwa katika miaka hiyo mnaenda kuomba kura tena kwa wananchi kama mlifanya vyema,” alisema Sumaye.

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, alisema sababu hizo hazina uzito kwani miaka mitano inatosha kupimwa na kama ulifanya vyema utaongezewa.

“Katiba yetu kwa sasa hairuhusu, lakini hatuwezi kusema kwa vile hairuhusu halijadiliki, lakini nasema ni kitu ambacho hakuna sababu hata ya kukisikia,” alisema Sumaye.

JUSSA

Kwa upande wake, Jussa alisema hizo zilikuwa ni njama zilizoanzia Bunge la Jamhuri ya Muungano na kupenyezwa Baraza la Wawakilishi.

Jussa ambaye kabla ya mgogoro amekuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Wananchi (CUF), alisema hoja hiyo ni sawa na ile iliyowahi kutaka kuwasilishwa bungeni na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), ya mabadiliko ya Katiba ili ……………..

Kwa habari kamili nunua nakala yako ya MTANZANIA

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles